Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wa Benki Ya Maendeleo Ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga (wa Pili Toka Kushoto) Akiwa Kwenye Picha Ya Pamoja Na Mwenyeji Wake Mkurugenzi Mkuu Wa Benki Ya Kilimo Ya Morocco (Credit Agricole) Bw. Jamal Eddine Wl Jamali (Katikati). Wengine Ni Mkurugenzi Wa Hazina Na Utafutaji Fedha Wa TADB  Bw. Albert Ngusaru Na Wakurugenzi Wawili Wa Benki Ya Credit Agricole Bi. Dkhil Mariem (Kushoto) Na Bi Leila Akhmisse (Kulia).

TADB YAANZA KUTEKELEZA MKATABA WA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA MOROCCO

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeanza kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Morocco wakati wa Ziara ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI alipotembelea Tanzania kwa mwaliko wa Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mnamo mwezi Oktoba 2016.

Katika kutekeleza makubaliano hayo, ujumbe wa TADB ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Francis Assenga na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru upo nchini Morocco, pamoja na mambo mengine kuainisha maeneo ambayo Benki hiyo itashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM) na kuwekeana mikakati ya utekelezaji.

Kwa mujibu wa Bw. Assenga, pamoja na kupanga mikakati hiyo, ujumbe huo ulipata fursa ya kukagua miradi kadhaa ya kilimo na ufugaji ambayo Tanzania inaweza kuianzisha kwa mafanikio.

TADB imeanzishwa kwa malengo makuu ya Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *